Huduma ya Kutafsiri Vitabu kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza

Swahili Book Translation Services

ProofreadingServices.com hutafsiri vitabu vya ubuni na visivyo vya ubuni kutoka lugha ya Kiswahili kwenda Kiingereza, hivyo huwasaidia waandishi kufikia wasomaji wapya pamoja na kuuza vitabu vingi zaidi. Huduma yetu ya kitaalamu ya kutafsiri hufanyika kwa kutumia binadamu kwa asilimia 100—kamwe hatutumii mashine za kiautomatiki—na tunajivunia utoaji wetu wa tafsiri sanifu huku tukihifadhi sauti na muundo wa uandishi wako.

Wasiliana nasi kujua gharama ya utafsiri wa uandishi.

Kwanini utafsiri kitabu chako kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza?

Umetumia miezi au hata miaka kuandika kitabu chako, sasa kwanini uzuie matokeo yake kwa kukichapisha kwenye lugha ya Kiswahili tu? Njia bora zaidi ya kuwafikia mabilioni ya watu ambao hawawezi kusoma lugha ya Kiswahili ni kutafsiri kazi yako kwenda Kiingereza. Kwa kutumia utaalamu wa utafsiri wa Kiingereza, utaongeza si tu wasomaji wako, bali pia mauzo yako.

Tunatoa huduma gani katika utafsiri wa vitabu?

Tunatoa huduma ya kutafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza cha Marekani au Kiingereza cha Uingereza, pamoja na kufanya uhakiki kupitia timu yetu ya Wazungumzaji Kiingereza. Wakati huduma nyingine zinatafsiri tu kitabu chako, sisi tunatafsiri uandishi huo pamoja na kuutuma kwa timu yetu ya wataalamu wa lugha ya Kiingereza ambao huondoa mikwaruzo yoyote ya maneno pamoja na kudaka makosa yoyote yaliyosalia. Kwani, ProofreadingServices.com ilianza ikiwa kama huduma ya kufanya uhakiki na uhariri, na timu yetu inajumuisha baadhi ya wahariri bora zaidi wa lugha ya kiingereza duniani.

Tunatafsiri uandishi ya namna gani?

Tunatafsiri riwaya, kazi zisizo za ubuni, vitabu vya watoto, na zaidi, kwa ajili ya waandishi kutoka pande zote duniani. Tumebobea katika…

  • Vitabu vya fasihi, kama vile riwaya za ubuni wa kisayansi, mafumbo, riwaya za mapenzi, na ubuni wa kihistoria
  • Vitabu vya taaluma, kama vile uandishi kuhusu falsafa, historia, sayansi, na maudhui nyingine
  • Vitabu vya biashara, kama vile vitabu vya kieletroniki kuhusu uzalishaji, vitabu vya dhamira za uongozi, na zaidi

Tumekwisha kufanya kazi na maelfu ya wateja ambao vitabu vyao vinahusisha mitindo na maudhui kadha wa kadha—kutoka ubuni wa vijana, hadi kwenye makala za kumbukumbu, vitabu vya mapishi, vitabu visivyo vya ubuni vinavyohusu sayansi ya siasa, teknolojia, na sanaa. Kwa kifupi, miaka yetu ya ujuzi ikijumuishwa na mtandao mpana wa wataalamu wa lugha inamaanisha kwamba, tunaweza kutafsiri pamoja na kufanya uhakiki wa karibu lugha yoyote, na kwenye maudhui yoyote.

Kwanini uchague huduma yetu ya utafsiri Kiswahili kwa ajili ya kitabu chako?

Katika ProofreadingServices.com, tunakabidhi vitabu kwa watafsiri wa fasihi, sio watafsiri wa kawaida. Mtafsiri wa fasihi mwenye ujuzi atavuka mipaka ya utafsiri wa neno-kwa-neno, na badala yake atazingatia kanuni za uandishi wako na kuhifadhi maana ndogo ndogo za sauti na muundo wa uandishi wako.

Tunakusudia kuwarahisishia waandishi kutoka pande zote duniani kuungana na watafsiri wenye viwango vya juu pamoja na wahakiki wa lugha ya Kiingereza. Iwe unaishi Nairobi, Dar es-Salaam, Mombasa, ama mahali pengine, huduma yetu ya kutafsiri Kiswahili-kwenda-Kiingereza pamoja na ufanyaji uhakiki ni njia rahisi ya kupata wasomaji wengi zaidi wa kitabu chako na kufurahia kazi yako. Tumejitoa kufikisha huduma ya utafsiri yenye kiwango-cha hali ya juu, na tunakuhakikishia kuwa utatoshelezwa na kazi yetu.

Wasiliana nasi kujua gharama ya utafsiri wa uandishi.