Huduma za Utafsiri wa Kitaalamu Mtandaoni
ProofreadingServices.com inatoa huduma ya kitaalamu ya kutafsiri Kiswahili kwenda Kiingereza, kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, na kwenye pea nyingine nyingi za lugha nyinginezo. Huku tukiwa tunatambulika vizuri kwa utoaji huduma zetu za ukaguzi na uhariri wa Kiingereza kwa ajili ya wanataaluma, watafuta ajira, wafanyabiashara, na waandishi kutoka pande zote duniani, huduma yetu ya utafsiri kupitia binadamu inaendelea kudumisha azimio letu la kutoa kazi zenye ubora wa hali ya juu, huduma safi kwa mteja, pamoja na gharama nafuu.
Wasiliana nasi kujua gharama ya kutafsiri.
Tunatoa huduma zipi za kutafsiri?
Je, unatafuta namna ya kuchapisha jarida la lugha ya kiingereza, kwenye nchi ya wazungumzaji kiingereza, ama vinginevyo? Tunatoa huduma ya kutafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza, pamoja na ufanyaji kaguzi uliotengwa na timu yetu ya Kiingereza.
Je, unataka kufikisha maudhui yako kwa mabilioni ya watu duniani, ambao hawazungumzi Kiingereza? Tunatoa huduma ya kutafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, Kiaislandi, Kislovenia, na zaidi.
Tumejikita katika …
- Utafsiri wa Kitaaluma. Waache timu yetu watafsiri nakala ya jarida lako, uandishi wa utafiti, tasnifu, kwenda Kiingereza ama kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili ili uweze kuchapisha kiupana zaidi na upanue wigo wa matokeo ya kazi yako.
- Utafsiri wa Kibiashara. Utafsiri wa tovuti ya kampuni yako, chapisho za blogu yako, dhana za masoko, pamoja na maudhui mengine ya biashara ni ufunguo wa kukuza biashara yako – pamoja na kutengeneza pesa nyingi zaidi.
- Utafsiri wa Kiandishi. Umefanya kazi kubwa kwenye muswada wako, iwe ni riwaya, kumbukumbu, au tamthiliya. Huduma ya kitaalamu ya utafsiri kwa kutumia binadamu unaweza kuongeza kwa kasi usomaji wa kazi yako pamoja na kuruhusu jukwaa la ulimwengu kufurahia kazi yako.
Kwenye ProofreadingServices.com, timu yetu ya wataalamu wa lugha imekwisha tafsiri maelfu ya nakala, na kuwatosheleza wateja huko Nairobi, Dar es-Salaam, na Mombasa pamoja na duniani kote. Tuna tofautiana na makampuni mengine ya kutafsiri kutokana na kwamba, sisi tunatoa huduma ya ufanyaji kaguzi wa Kiingereza sambamba na utafsiri wa Kiswahili-kwenda-Kiingereza ili kufanya nakala zilizotafsiriwa kuwa kama vile zimeandikwa na mzungumzaji mzawa.
Sisi ni nani?
Watafsiri wa ProofreadingServices.com wana ujuzi na uzoefu wa kutafsiri kwa usanifu kazi yako huku wakihifadhi muundo na lisani yako. Kwa kuwa watafsiri wetu wa Kiswahili wamebobea katika masomo kadha wa kadha—kutoka sheria hadi teknolojia—mradi wako utapatiwa kwa memba wa timu mwenye ufahamu na maudhui yako. Hivyo, ikiwa unahitaji chapisho la kitabu cha kielektroniki, pendekezo la utafiti, kutafsiriwa kutoka Kiingereza ama kwenda Kiingereza, unaweza kuwaamini timu yetu ya watafsiri wa Kiswahili kukuzalishia tafsiri ya mradi wako yenye ubora wa hali ya juu.
Kwanini uchague huduma yetu ya kutafsiri Kiswahili?
Kwenye ProofreadingServices.com, tunawarahisishia waandishi kutoka pande zote duniani kuungana na watafsiri wenye viwango vya juu pamoja na wafanya kaguzi wa Kiingereza. Huduma yetu sanifu na yenye gharama nafuu kwa ajili ya biashara, taaluma, pamoja na waandishi itakusaidia kuwafikia wasomaji wapya pamoja na kupanua ufikiaji masoko ya kimataifa, bila kujali lugha au mada. Tunajivunia ubora wa viwango vya juu unaofikiwa na wataalamu wetu wa tafsiri, na tunakuhakikishia kuwa utatoshelezwa na kazi yetu.